Tangaza Nasi

FAO: Maisha ya Watu Bilioni 2.5 hatarini kutokana na ukame


Ukame umesababisha hasara ya dola bilioni 29 kwa mataifa yanayoendelea na tegemezi kwa kilimo katika kipindi cha miaka 11 iliyopita, imesema ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Ripoti hiyo iliyozinduliwa Alhamisi huko Hanoi, Vietnam imeonyesha kuwa katika bara la Afrika, Amerika ya Kusini na visiwa vya Karibea ukame ndio balaa kubwa kwa kusababisha hasara ya mimea ya dola milioni 10.7 ilhali uharibifu wa mifugo ni dola bilioni 13. Hasara hiyo yote   ilitokea kati ya mwaka wa 2005 na 2015, imesema ripti ya FAO.

Ripoti ikionyesha kuwa watu takriban bilioni 2 na nusu duniani hutegemea kilimo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesema kuwa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, hukumbana na vizingiti vingi.

Ametaja vizingiti hivyo kuwa ni pamoja na hali ya hewa, soko lisilotegemewa, wadudu waharibifu, magonjwa na migogoro isiyoisha.
Kwa ujumla ukame pamoja na majanga mengine ikiwemo mafuriko, matetemeko ya ardhi, mmomonyoko wa udongo, vimbunga na moto yamesababisha jumla ya hasara dola bilioni 96. Bara la Asia limepata hasara ya dola bilioni 48 kutokana na majanga hayo yote.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.