Klabu zenye thamani kubwa Ulaya 2017, Top Ten hii hapa…
Washindi wa Europa League msimu wa 2016/17 Manchester United ya England imetajwa kuwa Klabu yenye thamani zaidi 2017 ikizipiku miamba ya La Liga Real Madrid na Barcelona zilizokamata nafasi ya pili na tatu. kwa mujibu wa KPMG.
Katika utafiti uliohusisha bei za matangazo, faida inayopatikana kwa mwaka, umaarufu, uwezo wa kimchezo na umiliki wa uwanja miongoni mwa klabu 32 za Ulaya, United imeibuka kinara kwenye list hiyo ikiwa na thamani ya euro 3.09b.
Nafasi ya pili inakamatwa na mabingwa wa La Liga Real Madrid yenye thamani ya euro 2.97b huku Barcelona wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya euro 2.76 ambapo katika Top Ten England imeingiza klabu Sita ikifuatiwa na Uhispania yenye timu Mbili huku Ujerumani na Italia zikiwa na klabu moja moja kila nchi.
Post a Comment