Tangaza Nasi

Mwakyembe Atuma Salamu Za Rambirambi Kifo Cha Mzee Kanyasu aliyechora nembo ya Taifa



 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali itaenzi michango yote ya wasanii wakongwe hapa nchini.

Ameyasema hayo kufuatia kifo cha mzee aliyebuni nembo ya taifa, Mzee Francis Kanyasu maarufu kwa jina la ‘Ngosha’ aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya kupatiwa matibabu.

“Tutaendelea kuwa karibu na familia ya marehemu Mzee Francis Kanyasu, kwani katuachia alama kubwa sana na mchango wake katika Taifa utakumbukwa milele”, amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo, katika kushiriki msiba huo, Mwakyembe atawakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza ambapo atakuwa akiiwakilisha Serikali.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.