Aliyeshika Kichwa Bandia cha Rais Trump Kikiwa Kimekatwa Kufunguliwa Mashtaka..!!!
Msanii mchekeshaji raia wa Marekani mwanamama Cathy Griffin alieonekana
live kupitia kipindi cha TV kinachorushwa na CNN akiwa ameshika kinyago
kinachofanana kabisa na kichwa cha rais Trump huenda akashtakiwa
kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya Uhuru wa habari.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 57 alionekana akiwa amebeba kinyago cha
Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, Jambo ambalo limezua hasira miongoni
mwa watu wengi wakiwemo wapinzani wa Trump nchini marekani.
Baada ya Tukio hilo Kituo cha TV cha CNN kilitangaza kumfukuza kazi msanii huyo na kukifuta kipindi chake mara moja
Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo rais Trump mwenyewe
wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa
familia za Wanajeshi na baadhi ya waandishi wa habari wa Marekani
waliochinjwa na Kikundi cha kigaidi cha ISIS
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi wa Rais nchini marekani (Secret
Service) imesema uchunguzi umekamilika na wanajiandaa kumfikisha
mahakamani Cathy Griffin.
Post a Comment