Tangaza Nasi

Bilioni 3 kusaidia watoto wa kike

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetenga dola za Marekani 1,605,000 (zaidi ya Sh. bilioni 3) kusaidia watoto wa kike nchini kurejea shuleni.


Takwimu ya mwaka (2015) kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania zinaonesha kuwa mikoa inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni ni Shinyanga ambayo ina asilimia 59 ya ndoa za utotoni.

Mikoa mingine ni Tabora 58, Mara 55, Dodoma 51, Lindi 48, Mbeya 45, Morogoro 42, Singida 42, Rukwa 40, Ruvuma 39, Mwanza 37, Kagera 36, Mtwara 35, Manyara 34, Pwani 33, Tanga 29, Arusha 27, Kilimanjaro 27, Kigoma 29, Dar es salaam 19 na Iringa asilimia 8.

Tanzania bado kuna tatizo la watoto wa kike kuachishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba za utoto na ndoa za utotoni hivyo kupitia mradi huo wataweza kuwasaidia watoto hao kuendelea na masomo.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.