Tangaza Nasi

Bunge laidhinisha Mfalme kung'atuka

 
Bunge la Japan limeidhinisha sheria itakayomuwezesha Mfalme wa nchi hiyo Akihito kuondoka madarakani, jambo ambalo litakuwa la kwanza kwa mfalme kung'atuka nchini humo kwa zaidi ya miaka mia mbili.

Zoezi la upigaji kura katika bunge la juu, limeoneshwa moja kwa moja na Televisheni.

Sheria hiyo mpya ilianza kupitishwa na bunge la chini wiki iliyopita.

Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 83 aliishangaza nchi hiyo, mwaka uliopita kwa kuelezea nia yake ya kung'atuka, kutokana na afya yake na umri.
Mwana wa Mfalme Naruhito anatarajiwa kushika nafasi hiyo


Jiunge na BongoTune sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune!

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.