Tangaza Nasi

Cristiano Ronaldo kutimkia Manchester United

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ametishia kuondoka katika klabu hiyo baada aya kuandamwa na vyombo vya  sheria vya nchini Hispania.

Ronaldo mewnye umri wa miaka 32 amesema hataki tena kukaa katika nchi hiyo na upo uwezekano mkubwa wa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United.

Mapenzi aliyonayo kwa klabu hiyo,uwepo wa kocha mreno mwenzake Jose Morinho  na ukweli kwamba Manchester United ndio klabu iliyokuza kipaji chake zinaweza kuwa sababu za kumrudisha Ronaldo Old Trafford.

Ramon Calderon ni raisi wa zamani wa Real Madrid na kwa uzoefu wake wa soka na kuishi na wanamichezo wakubwa dunia amekiri kwamba pamoja na uwezo wa kifedha wa Real Madrid lakini ni ngumu kumzuia Ronaldo kuondoka katika klabu hiyo kama akitaka kufanya hivyo.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.