Tangaza Nasi

Eden Hazard: Nyota wa Chelsea asema anaweza 'kuwasikiliza' Real Madrid

Winga wa Chelsea Eden Hazard amesema anaweza 'kusikiliza' Real Madrid wakiwasilisha ombi la kumnunua, lakini akaongeza kwamba atasalia na The Blues "kwa miaka mingi".

Hazard ambaye aliumia kwenye kifundo chake cha mguu akifanya mazoezi na timu ya taifa ya Ubelgiji amekuwa akihusishwa sana na kuhamia Madrid, kwa klabu hiyo iliyoshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
"Sote huwa tuna ndoto. Inaweza kuwa Uhispania, lakini inaweza pia ikawa kusalia na Chelsea," aliambia gazeti la Het Laatste Nieuws.
"Lakini si jambo ambalo nalifikiria wka sasa. Tutasubiri tuone."

Real walilaza Juventus 4-1 na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa kwa mara ya 12 Jumamosi.

Hazard aliongeza: "Ikitokea kwamba nihamie Real Madrid, kuna uwezekano ninaweza kuwekwa kwenye benchi pia. Ninataka uamuzi bora zaidi kwangu."

Hazard, 26, alijiunga na Chelsea akitokea Lille ya Ufaransa Juni 2012 na kuwasaidia Chelsea kushinda Ligi ya Premia msimu uliomalizika majuzi.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuihama Chlsea, alisema: "Katika soka, huwezi ukajua, lakini sasa hilo halimo akilini mwangu.
"Mimi ni mchezaji wa Chelsea. Bado nimesalia na miaka mitatu katika mkataba wangu. Tutasubiri."

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.