Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wadau wa sekta ya utalii mkoani humo kujadili namna mbalimbali wanazoweza kuboresha sekta ya utalii mkoani humo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kutaka kuliboresha jiji la Arusha sekta ya utaliii

Gambo amesema jiji hilo linatakiwa kuwa hali nzuri hasa katika mazingira ya utalii kwani linachangia asilimia 80 katika sekta hiyo.
“Mkoa wa Arusha unachangia mapato ya utalii nchini kwa zaidi ya asilimia 80 hivyo sisi kama mkoa tukiwa na mikakati madhubuti ya kuiboresha hii sekta tutakua tumeikuza sekta hii kiasi cha kuleta matokeo chanya kwa taifa kiujumla.” Amesema Gambo.

Hata hivyo kwa upande wao wafanyabiashara wa utalii (TATO) wamesema changamoto katika biashara hiyo ni nyingi lakini kwa sehemu kubwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutatua asilimia kubwa ya changamoto hizo.