Je nguo za kubana zina madhara kwa mwili wa binaadamu?
Je, ni kweli mitindo mipya au........
Kumekuwa na tishio kwamba vitu vya
mitindo huenda vikaathiri maungo ya mwili wa mwanadamu hususan mgongo
mbali na matatizo ya shingo.
Muungano wa Uingereza wa madaktari wa kutibu matatizo ya viungo BCA unasema kuwa vitu kama jinsi zinazobana, viatu vya juu na mikoba ya wanawake huathiri mwili.
Hatahivyo utafiti huo umekataliwa na muungano wa watabibu wa viungo nchini humo na wataalam wengine.
Wanasema hatufai kuogopa nguo zetu.
Hivi ndio vitu vitano ambavyo muungano wa madaktari wa kutibu maungo ya mwili unasema vinaweza kutusababishia madhara.
Muungano huo unadai kwamba jinsi zinazobana zinapunguza mwendo wa mtu hata iwapo ni kutembea tu.
''Nguo zinazokubana hukufanya kushindwa kuruka unapotembea na kudhibiti mwendo wako na hivyobasi kusababisha shinikizo katika viungo''.
Muungano huo wa matabibu unasema kuwa mabegi ya mikononi ndio sababu kuu ya maumivu ya mgongo miongoni mwa wanawake.
Wanasema kuwa tunapaswa kuzuia kutumia mabegi ambayo yanafaa kubebwa katika mabega, kwa kuwa uzito wake husababisha bega moja kuzama upande mmoja .
Vilevile muungano huo unasema kuwa mabegi mazito ndio sababu kuu ya maumivu ya mgongo miongoni mwa wanawake.
BCA inadai kwamba viatu vya juu hutufanya kubeba miili yetu katika njia ambayo husababisha shinikizo fulani katika uti wa mgongo.
Unasema kuwa nyumbu hukosa uthabiti nyuma ya mguu swala ambalo husababisha shinikizo katika miguu na chini ya uti wa mgongo.
Pia wameonya kwamba mavazi yenye mitindo mipya kama yale yenye vito, mavazi makubwa au mazito kupitia kiasi pia yanaweza kumsababishia matatizo anayevaa.
Kura ya maoni iliofanyiwa watu 1,062 ilibaini kwamba asilimia 73 walipatikana na matatizo ya mgongo huku asilimia 33 ikiwa hawajui kwamba nguo zinaweza kuathiri migongo yao ,shingo ama hata maungo yao.
Wameonya kwamba nguo zozote zinazothibiti mwendo na kumfanya mtu kusimama ama kutembea vibaya zinaweza kuathiri maungo ,mgongo ama hata shingo.
"Ushauri ni kuangazia afya ya mgongo ama hata shingo wakati mtu anapotafuta nguo ya kuvaa ama hata kununua''.
Nguo zisizodhibiti mwendo wako zinafaa. Lakini Dkt Mary O'Keefee ambaye ni mtaalam wa maswala ya mgongo katika chuo kikuu cha Limerick anasema kuwa utafiti huo ni wa uzushi na hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kuunga mkono.
Kuvaa mavazi ya kawaida yanayobana , mikufu pamoja na nguo nyengine zozote hakusababishi maumivu ya mgongo.
Hakuna ushahidi wowote wa muungano.
Hii sio ukweli kwa sababau wanawake wenye matatizo ya mgongo wanaweza kusema kuwa wana maumivu ya mgongo wakati wanapovaa ama hata kubeba vitu fulani.
Hatahivyo, kudai kwamba maumivu ya mgongo husababishwa nguo hizo ni sawa na kumweka farasi nyuma ya mkokoteni.
Post a Comment