Majeshi ya Congo Brazzaville yatakiwa kuondoka CAR
Kamanda wa majeshi ya kulinda amani nchini
Jamahuri ya Afrika ya Kati anataka vikosi kutoka Congo Brazzaville
kuondolewa nchini humo, kutokana na vitendo vya aibu wanavyofanya.
Luteni Jenerali Balla Keita amesema wanajeshi wa Congo wameendelea kutuhumiwa kuhusika katika unyanyasaji wa kimapenzi, biashara haramu ya mafuta na nidhamu yao sio ya kuridhisha.
Mwaka uliopita, wanajeshi 120 wa nchi hiyo walirejeshwa nyumbani baada ya kubainika kuhusika katika makosa hayo. Nchi hiyo imetuma wanajeshi 750 katika kikosi hicho cha MINUSCA.
Majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati yamekua yakilaumiwa kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi.
Baadhi ya askari kutoka Ufaransa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na wengine kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika walihusishwa katika vitendo hivyo.
Post a Comment