Man Utd Yarejea Kileleni, Yaibwaga Real Madrid
Klabu ya Man Utd imerejea kileleni mwa klabu zenye thamani kubwa ya
utajiri duniani na kuwapiku mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hii leo jarida la Fobes la Marekani, klabu hiyo ya Old Trafford imekuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 3.69 sawa na Pauni bilioni 2.86.
Hii inakua ni mara ya kwanza baada ya miaka mitano kupita kwa Man Utd kurejea kileleni mwa orodha ya klabu zenye thamani kubwa ya tajiri duniani.
Real Madrid ambao ni mabingwa wa soka barani Ulaya na Hispania waliwahi kuwa vinara katika orodha hii kwa miaka minne mfululizo iliyopita, lakini kwa mwaka huu wameshuka kwa asilimi mbili huku Man Utd wakipanda kwa asilimi 11 ya thamani ya utajiri wao.
FC Barcelona wanashika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.64 sawa na Pauni bilioni 2.82 na Real Madrid ipo nafasi ya tatu kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.58 sawa na Pauni bilioni 2.77.
Katika kumi bora ya orodha hiyo England imeingiza klabu sita ambazo ni Manchester City, Arsenal, Chelsea, Liverpool, Tottenham na Man Utd.
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku mabingwa wa Italia Juventus wakiangukia nafasi ya tisa.
Orodha iliyotolewa hii leo na jarida la Forbes la Marekani inayoonyesha thamani ya utajiri wa klabu 20 za soka duniani.

- Manchester United $3.69bn (£2.86bn)
- Barcelona $3.64bn (£2.82bn)
- Real Madrid $3.58bn (£2.77bn)
- Bayern Munich $2.71bn (£2.1bn)
- Manchester City $2.08bn (£1.61bn)
- Arsenal $1.93bn (£1.5bn)
- Chelsea $1.85bn (£1.43bn)
- Liverpool $1.49bn (£1.15bn)
- Juventus $1.26bn (£976m)
- Tottenham $1.06bn (£821m)
- Paris St-Germain $841m (£652m)
- Borussia Dortmund $808m (£626m)
- AC Milan $802m (£621m)
- Atletico Madrid $732m (£567m)
- West Ham $634m (£491m)
- Schalke 04 $629m (£487m)
- Roma $569m (£441m)
- Inter Milan $537m (£416m)
- Leicester City $413m (£320m)
- Napoli $379m (£294m)
Post a Comment