Tangaza Nasi

Moto mkubwa watishia mji wa Knysna, Afrika Kusini

Nchini Afrika ya Kusini, baada ya dhoruba iliopiga katika mkoa wa Cape wiki hii, na kuua watu wasiopungua tisa, moto mkubwa uunaukumba tangu siku ya Jumanne mji wa Knysna. Maelfu ya watu tayari wameondolewa katika mji huo.

Tangu Jumatano alasiri, takriban watu 10,000wamehamishwa kutoka mji wa Knysna, mji wa kitalii uliyoko kilomita 400 kutoka mji wa Cape Town na unazungukwa na hifadhi za taifa. Moto huu unaendelea kushika kasi. Upepo ni mwingi kwa sababu ya dhoruba inayoendelea kuukumba mkoa huo na maafisa wa idara ya zima moto wameshindwa kudhibiti motohuo. Pia haiwezekani kutumia helikopta kupambana dhidi ya moto huo.

Alhamisi asubuhi, moto huo ambao ulikua hasa katika milima karibu na mji wa Knysna, ulikua ukikaribia katika eneo la kati la mji huo. Barabara zinazoingia katikati mji wa Knysna zimefungwa na askari 150 walitumwa kuzuia majambazi kupora mali za raia mbalimbali. Watu tisa wamearifiwa kupoteza maisha siku ya Alhamisi na nyumba kadhaa kuteketezwa kwa moto.

Jeshi la Taifa la Afrika Kusini litasaidia kuangusha mabomu ya maji yanayotumiwa kuzima moto kusaidia kukabili moto huo, msemaji wa jeshi Simphiwe Dlamini amesema.


Jiunge na BongoTune sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune!

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.