Tangaza Nasi

Qatar yatupilia mbali masharti ya Mataifa ya kiarabu

     Waziri wa mambo ya kigeni wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahm
      - ---------------------------------------------------------------------------------------------
Nchi ya Qatar imetupilia mbali masharti kadhaa yaliyotolewa na mataifa manne ya kiarabu kwa kile ilichosema hayana msingi wala hayatekelezeki.

Orodha hiyo ya masharti ilipokelewa na wizara ya mambo y akigeni ya Qatar mnamo June 22, kwa mujibu wa shirika la habari nchini humo.

Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano nchini Qatar Sheikh Saif bin Ahmed Al Thani,amesema orodha hiyo y amasharti inathibitish akile Qatar ilikisema tangu awali kuwa zuio lisilo la kihalali dhidi ya Qatar halikulenga kupambana na ugaidi bali kuzuia uhuru wa Qatar na kuingilia sera za mambo ya kigeni za Qatar.

Masharti 13 ambayo Mataifa manne ya kiarabu yaliitumia Qatar yalitaka iafiki iwapo inataka kuondolewa vikwazo,kwa mujibu wa vyombo vya habari

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.