Real Madrid yampiga bei mtoto wa Zidane
REAL MADRID imeanza kuondosha watumishi hewa kwenye kikosi chake cha
kwanza hii ni baada ya Jana usiku kumuuza kiungo wake,Enzo Zidane kwenda
klabu ya Deportivo Alaves kwa ada ya uhamisho ambayo imefanywa siri.
Enzo ,22, ambaye ni mtoto wa kwanza wa kocha, Zinedine Zidane amejiunga
na Deportivo Alaves kwa mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha
kurejea tena Real Madrid iwapo atahitajika hapo baadae.
Enzo anaihama Real Madrid akiwa amefanikiwa kuicheza mchezo mmoja pekee
msimu uliopita tena ikiwa dhidi ya Cultural Leonesa kwenye mchezo wa
kombe la mfalme ambapo alifunga bao moja.
Sehemu kubwa ya soka la Enzo limekuwa kwenye kikosi cha pili cha Real
Madrid cha Castilla ambacho amekichezea michezo 78 na kufunga mabao
saba.

Post a Comment