Sakho wa liverpool atua moshi kupanda mlima kilimanjaro
BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kiutalii.
Sakho
ameonekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo
na inafikiriwa anakwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Mchezaji
huyo anaonekana Tanzania siku mbili tu baada ya Nahodha na kiungo wa
zamani wa kimataifa wa England, David Beckham kuondoka nchini kufuatia
wiki moja ya kutalii kwenye vivutio mbalimbali, ikiwemo mbuga ya wanyama
ya Serengeti.
Mamadou
Sakho (katikati) akiwa na wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili kwa ziara ya utalii
Sakho
aliyezaliwa Februari 13, mwaka 1990, kisoka aliibukia Paris FC kabla ya
kuhamia timu ya vijana ya Paris Saint-Germain mwaka 2002 na Oktoba
mwaka 2007 aliweka rekodi ya mchezaji kijana daima kuiongoza timu hiyo
kam Nahodha katika Ligue 1.
Sakho
amecheza mechi zaidi ya 200 katika klabu hiyo, akishinda nayo mataji
yote manne ya nyumbani kabla ya mwaka 2013 kuuzwa Liverpool kwa dau la
Pauni Milioni 18.
Mwaka huu alitolewa kwa mkopo Crystal Palace pia ya Ligi Kuu England ambako amekwenda kucheza mechi nane.
Sakho ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wakubwa cha Ufaransa, ambaye awali amechezea timu zote za vijana na za nchi hiyo.
Sakho ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wakubwa cha Ufaransa, ambaye awali amechezea timu zote za vijana na za nchi hiyo.
Tangu
acheze mechi yake ya kwanza kikosi cha wakubwa cha Ufaransa mwaka 2010
dhidi ya England, Sakho amecheza mechi zaidi ya 25 na alikuwemo kwenye
kikosi cha timu hiyo kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini
Brazil.
Huyo ni mume wa Majda, ambaye amezaa naye watoto wawili wa kike, waliozaliwa mwaka 2013 na 2015.
Post a Comment