Tangaza Nasi

Salah aweka rekodi mpya ya usajili Liverpool


Salah amepewa jezi namba 11 aliyokua akivaa Roberto Firmino ambae kwa sasa atavaa jezi namba 9 Liverpool wamekamilisha dili la usajili winga Mohamed Salah, kutoka As Roma ya Italia, kwa dau la Pauni million 39.

Usajili wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2011.

Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuweza kutumikia Liverpool.

“Ninafuraha sana kuwepo hapa nitajitoa kwa asilimia mia moja na nitatoa kila kitu kwa ajili ya klabu hii, kiukweli nataka kushinda kitu nikiwa na timu hii”, alisema Salah baada ya kukamilisha usajili huo.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.