Southampton wamfuta kazi meneja Claude Puel

Southampton pia walifika fainali ya kuwania Kombe la Ligi, mara yao ya kwanza kucheza fainali kubwa tangu 2003.
Taarifa ya Southampton imesema: ''Mipango ya kutafuta timu mpya ya usimamizi inaangaziwa. Tuna uhakika kutapata watu wanaostahili, wenye mitazamo ya kudumu.''
Puel alihudumu kwa miaka minne kama meneja wa Nice kabla ya kuchukua nafasi ya Ronald Koeman, aliyeiongoza Southampton kumaliza katika nafasi ya sita katika jedwali msimu wa 2015-16
Southampton walichapwa mabao 3-2 na Manchester United katika fainali ya Kombe la Ligi iliyochezwa mwezi Februari.
Walipata ushindi mmoja katika michezo yao minane ya mwisho katika ligi na kufunga goli moja katika michezo yao sita ya mwisho.
Taarifa ya Klabu hiyo: ''Kila mmoja Southampton angependa kutoa shukurani zetu kwa Claude kwa bidii yake na jitihada zake mwaka huu.
''Kitu cha kukumbuka msimu huu ni katika uwanja wa Wembley katika fainali ya EFL siku ambayo mashabiki wataikumbuka siku zote.''
Puel ni meneja wa tatu kuiaga Southampton kwa miaka mitatu iliyopita, baada ya Mauricio Pochettino kuhamia Tottenham na Koeman kuelekea Everton.
Meneja huyo wa zamani wa Monaco alipigwa kalamu mwaka mmoja baada ya Koeman kuiaga klabu hiyo mwezi Juni mwaka 2016.
Puel aliteuliwa tarehe 30 mwezi Juni, 2016 na inaaminika kwamba watakatifu hao wa St Mary's wanasubiri wakati kama huo kumtaja meneja wa mpya.
Post a Comment