Uganda yaiomba radhi China kwa madai ya kuhusika na biashara ya pembe za ndovu
Serikali ya Uganda imeiomba radhi serikali ya
China, baada ya Beijing kukataa madai kuwa wafanyikazi wake wawili
wanaofanya kazi katika Ubalozi wake jijini Kampala, walihusika katika
biashara haramu ya pembe za ndovu.
Mapema mwezi huu rais Yoweri
Museveni alinukuliwa katika vyombo vya Habari nchini mwake, akitaka
uchunguzi kufanyika kubaini ukweli wa ushirikiano wafanyikazi hao na
wale wa Shirika la kuhifadhi Wanyama Pori nchini humo baada ya
kutowekakwa Kilo 1,300 za pembe za ndovu.
Wizara ya Mambo ya nje ya Uganda imesema inasikitika kwa namna madai hayo yalivyoichafulia jina Ubalozi wa China na kusisitiza kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili haujatikiswa.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Patrick S. Mugoya amesema baada ya uchunguzi wa kina, wamebaini kuwa taarifa za wajumbe wa ubalozi wa China ambao wamebainika kuwa ni Li Wejin na Yinzhi walikuwa si wafanyikazi wa Ubalozi huo kama wajumbe.
China mwaka uliopita, ilitangaza kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu, itapiga marufuku uingizwaji wa pembe za ndovu nchini humo.
Uganda imeendelea kunufaika pakubwa sana na msaada wa kifedha na mkopo kutoka nchini China, kwa lengo la kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama barabara na majengo.

Post a Comment