Tangaza Nasi

Wachezaji wa Serengeti Boys watafutiwa nafasi Everton




Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara yake iko katika mazungumzo na wadau wa michezo kutoka nje ikiwemo klabu ya Everton ili kuishawishi iweze kuwachukua baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys. 

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto lililohoji jitihada za serikali za kuwawezesha vaijana hao kupata nafasi katika timu za nje ya nchi zinazofanya vizuri kwenye ligi mbalimbali duniani, katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.

“Timu yetu imefanya vizuri sana katika historia ya nchi yetu, juhudi ya serikali ni pamoja na kuhakikisha timu hii tunaendelea kuilea sababu hawa ni wawakilishi wetu wa mashindano ya Olimpic 2020, pia tuko katika mazungumzo na wadau wa nje Sportpesa na Everton tumeongelea kuhusu uwezekano wa uwachukua vijana wetu. Sitaruhusu kijana kwenye timu ya Serengeti achukuliwe na timu yenye uchovu wa pesa na matokeo mazuri,” amesema.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.