Wanyama hatarini kupotea Mto ruaha mkuu
WANYAMAPORI waishio katika maji ya mto Ruaha mkuu eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa, wapo hatarini kupoteza maisha baada ya maji ya mto unaopita ndani ya hifadhi ya Ruaha kuendelea kupungua- hali ambayo imetajwa kuwa ni hatari kwa usalama wa wanyamapori na viumbe mbalimbali viishivyo katika mto huo.
Hayo
yamezungumzwa na Epaphras Muse- Daktari wa wanyamapori kutoka katika hifadhi ya
Ruaha mkoani Iringa, ambaye amesema wanyamapori wanaoishi katika maji kama Samaki,
Mamba, Viboko wapo hatarini mara maji hayo yatakapokauka.
Aidha Dokta Muse
amesema licha ya wanyama wote hifadhini kuathiliwa na changamoto ya kupungua
kwa maji hayo ya mto Ruaha, lakini athari kubwa nikwa wanyama, wadudu na viumbe
hai mbalimbali ambavyo vinaishi ndani ya maji
Naye Rodrick Mpogolo naibu katibu mkuu wa
chama cha mapinduzi CCM Tanzania Bara, aliyefika
katika hifadhi hiyo ya Ruaha kuona mazingira namna yalivyo, amesema kila
mtanzania anao wajibu wa kutunza mazingira ili kuunusuru mto Ruaha mkuu ambao
unategemewa katika sekta ya uchumi.
Mpogolo
amezitaka wizara zinazotegemea maji kukaa kwa pamoja na kutafuta namna njema ya
kuuokoa mto huo ambao ni rasilimali ya sekta ya Maliasili na utalii, Nishati na
madini, Kilimo na umwagiliaji pamoja na sekta ya Mifugo.
Awali katika uzinduzi
wa kikosikazi cha kuokoa mazingira ya mto Ruaha mkuu, ambacho kilizinduliwa
rasmi na makamu wa rais Samia Hassan Suluhu mkoani Iringa - aliitaka jamii kuwa
rafiki wa mazingira kwakutunza vyanzo vya maji ili dunia iwe ni sehemu saklama
ya kuishi.
Na mwandishi wetu
Oliver Motto
Post a Comment