Tangaza Nasi

Korea Kaskazini yarusha kombora jingine la masafa marefu


Taarifa kutoka jeshi la Korea Kusini, zinabaini kwamba "kombora la masafa marefu lisilojulikana" lilirushwa kutoka eneo lililo karibu na mkoa wa Banghyon, magharibi mwa Korea Kaskazini.

Kombora hilo lilianguka katika Bahari ya Japan, kwa mujibu wa taarifa hizo.
Kombora hilo lililorushwa Jumanne hii lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40, kulingana na taarifa kutoka Korea Kusini na Japan.

Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika miezi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua hali ya sintofahamu.

Korea Kaskazini imeendelea na majaribio yake wakati ambapo Umoja wa Mataifa na Maekani wameendelea kuionya kutoendelea na mpango wake huo.

Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.

Wakati huo rais mpya wa Korea Kusini ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano wa dharura kuhusu swala hilo.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.