Tangaza Nasi

Lukaku akataa ndoa na Chelsea: Arudi mikononi mwa Mourinho


Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Klabu ya Everton, Romelu Lukaku kwa ada ya Euro Milioni 75 .

Hii ni kufuatia dili la alavaro moratta kushindikana 

Lukaku aliyekuwa akiwindwa na Klabu yake ya zamani ya Chelsea ameitolea nje klabu hiyo na kuamua kurudi mikononi mwa kocha wake wa zamani, Jose Mourinho ambaye anakinoa kikosi cha Manchester United kwa sasa.

Usajili wa Lukaku ndani ya Manchester United unaongeza joto kwa Wayne Rooney ambaye kwa siku mbili mfululizo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuihama klabu hiyo na kurudi Everton.
Wakati huo huo Klabu ya Manchester United ipo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata .

Kwa mujibu wa Gazeti la Marca taarifa zinasema Morata yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester United ingawaje Wakala wake anahitaji kiasi cha Euro milioni 90 wakati hao Man united wapo tayari kulipa kiasi cha Euro Milioni 79.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.