Ray C kukesha studio siku mbili
Msanii wa Bongo Flava na hitmaker wa ngoma ‘Unanimaliza’, Ray C
inaelezwa kutokana na uwezo wake wa kazi si ajabu yeye kukesha studio
siku mbili akifanya kazi.
Mmoja wa mameneja wake, T Fighter ameeleza kwa malezi aliyolelewa Ray
C ni tofauti na wasanii wengine kwani amezoea kurekodi albamu na si
single.
“Tukienda studio tunakesha hata siku mbili, mimi nishazoea nikienda
studio nakaa lisaa limoja naondoka ila yeye akiingia studio anakaa siku
mbili anarekodi nyimbo tatu au nne kali,” ameiambia Planet Bongo ya EA
Radio.
Ameongeza kuwa kutokana na uwezo wake wa kazi wimbo wa Unanimaliza ulirekodiwa ndani ya saa mbili tu.


Post a Comment