Tangaza Nasi

Je Mo Salah anakaribia kumrithi Messi?


Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa Mohamed Salah anakaribia kulinganishwa na Lionel Messi baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Watford.
Salah ndiye anayeongoza kwa mabao katika ligi tano bora za Ulaya akiwapiku Lionel Messi wa Barcelona na Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane.
Lakini kulingana na Klopp mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Misri ananedelea vyema.
''Sidhani kwamba Mo anataka kufananishwa na Lionel Messi'', alisema.
''Messi amekuwa akifanya kile anachofanya kwa zaidi ya miaka 20 iliopita'' .
Machezaji wa mwisho aliyekuwa na ushawishi kama huo kwa timu yake alikuwa Diego Maradona.
Akiwa na umri wa miaka 25 Salah ana kibarua kigumu kuafikia yale yalioafikiwa na Messi.
Alishiriki katika mechi tatu za ligi ya Uingereza akiichezea Chelsea wakati ambapo klabu hiyo ilishinda ubingwa wa ligi 2015, pia alikuwa miongoni mwa kikosi cha Basel cha 2012 na 2014 wakati klabu hiyo iliposhinda mataji ya ligi.
Winga huyo pia aliisaidia Misri kushiriki katika kombe la dunia baada ya robo karne wakati alipofunga bao la dakika 95 kwa njia ya penalti katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Congo.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.