Prezzo afunguka kutompost Amber Lulu kwenye ‘birthday’ yake
Prezzo ameweka wazi sababu iliyosababisha kutompost aliyekuwa mpenzi wake, Amber Lulu kwenye Instagram alipokuwa akiadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Rapa huyo ambaye jana aliitembelea FNL ya East Africa TV alisema kuwa hakuona sababu ya kufanya hivyo kwani sio ishara ya kuonesha kuwa unampenda mtu fulani.
“Sio lazima umpost mtu Instagram ndio wajue unampenda. Kwani birthday ngapi zimepita lakini mama yangu hajanipost?” Prezzo alifunguka, huku akikataa kuzungumzia sababu za kuachana na mrembo huyo.
Post a Comment