Tangaza Nasi

Video: Goodluck Gozbert aachia ngoma mpya ”Hauwezi kushindana”

Msanii wa nyimbo za Injili, mwandishi mzuri wa mashairi ya muziki, na mkali wa nyimbo ya Ipo siku, Goodluck Gozbert ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ”Hauwezi Kushindana”.
Wimbo huo wenye ujumbe mzito unaendelea kukonga mioyo ya mashabiki wengi ambao wanafuatilia na kusikiliza muziki mzuri wenye mashairi mazuri yaliyoandikwa na mtunzi huyo.
Goodluck Gozbert ni moja kati ya vijana waimbaji wazuri wa muziki wa injili ambao wameinua muziki huu na kuuletea mtazamo tofauti.
Kufuatia muziki wake wenye mvuto amesisimua na kuibua vijana wengi kuufanya muziki huo ambao huko nyuma ulidhaniwa kuwa ni muziki wa watu wazima, ujio wa Goodluck Gozbert umeleta tofauti sana katika muziki wa injili.
Kuusikiliza wimbo huo bonyeza linki hapo chini ili kuangalia video ya wimbo huo unaofanya vizuri kwa upande wa nyimbo za injili.                   

                     




Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.