Wafanyakazi wapenda kazi kupita kiasi kufukuzwa wakapumzike Korea Kusini
Serikali nchini Korea Kusini imeanzisha mpango wa kuwalazimisha wafanyakazi kuondoka kwa wakati baada ya kumalizika kwa zamu yao.
Mpango huo unahusisha kuzimwa kwa lazima kwa kompyuta za wafanyakazi hao afisini saa mbili usiku kila Ijumaa.
Lengo la mpango huo ni kujaribu kufikisha kikomo "utamaduni wa kufanyakazi muda wa ziada".
Wafanyakazi nchini humo hufanya kazi muda mwingi zaidi kwa siku ukilinganisha na wafanyakazi wengine nchi nyingine duniani.
Wafanyakazi wa serikali Korea Kusini kwa kawaida hufanya kazi saa 2,739, muda ambao ni saa 1,000 zaidi ya muda wanaofanya kazi watumishi wa umma katika mataifa yaliyoendelea.

Post a Comment