Tangaza Nasi

ATCL kufungiwa kwa kudaiwa Mabilioni

Shirika la Ndege nchini ATCL limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga IATA kutokana na kukabiliwa na madeni na sasa limetia saini makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya Ndege ya HAHN Air kuuza tiketi za Air Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari visiwani Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi amesema wamelazimika kuingia makubaliano na kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma ya malipo ya tiketi.
“Sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa, ambayo yalisababisha siye kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka tutakapokuwa tumelipa hayo madeni” -Matindi
“Kubwa zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa Shirikisho la Mashirika ya ndege ya Dunia IATA, ambao kwa kweli ni sehemu mojawapo ya huo mfumo wote wa utawanyaji na uuzaji wa ticket, maana mabadilishano ya pesa au upelekaji wa pesa kutoka shirika moja kwenda lingine upitia IATA, ni kupitia mgongoni kwa mtu, lazima tutoe madeni yetu tuliyonayo IATA na ni Mabilioni” -Matindi

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.