Tangaza Nasi

Neymar arudi uwanjani kwa mbwembwe, tazama mazoezi yake ya kwanza akiwa na PSG (+video)

Kama wewe ni mshabiki wa timu ya taifa ya Brazili na unamkubali sana mshambuliaji wa klabu ya Paris St. Germain  basi habari hii nzuri kwako.

Neymar Jr
Mshambuliaji wa klabu ya PSG, Neymar Jr tayari ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza cha PSG na ni uhakika wa asilimia 98 kuwa mshambuliaji huyo atacheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini Urusi.
Wiki mbili zilizopita Neymar Jr alikuwa anafanya mazoezi peke yake kitu ambacho kilianza kuibua maswali mengi kuhusu ushiriki wake kombe la dunia.
Neymar Jr aliumia kifundo cha mguu mwezi Februari mwaka huu na kurudishwa kwao Brazili kwa ajili ya matibabu. Tazama video akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa PSG hapa chini.
                     



Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.