Tangaza Nasi

Panya watano wafikishwa polisi kwa kula pesa

Mfanyibiashara mmoja kutoka nchini Uganda amewapeleka panya watano katika Kituo cha Polisi cha Kotido Central katika tukio la kushangaza lililowaacha wanakijiji wenzake midomo wazi.
Peter Lojok Longolangiro aliwatuhumu ‘watuhumiwa ’ watano kwa kuharibu pesa zake alizokuwa ameweka ndani ya sanduku.
Mtandao wa Watchdog Uganda, umesema Longolangiro alidai kuwa panya hao walikula fedha za kenya  KSh 10,000 sawa na shilingi 227404 za kitanzania, ambazo alifikisha mbele ya  kituo cha polisi kama ushahidi. 

Mfanyibiashara huyo pia alilishtaki shirika la kulinda wanyamapori la Uganda kwa kushindwa kulinda wanyama wake. Alidai kuwa panya hao waliingilia faragha yake na kuingia ndani ya kisanduku hicho alichokuwa amehifadhi akiba yake na kuharibu pesa hizo. 
Kamanda wa Polisi wa eneo hilo Alphonse Ojangole, alimpa idhini Longolangiro kuwasilisha kesi hiyo mbele ya Mwanasheria Mkuu ili apokee mwelekeo wa kitaalam kuhusiana na kisa hicho. Ojanjole alisema hajawahi kukabiliwa na kesi ya aina hiyo licha ya kufanya kazi kama polisi kwa miaka mingi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.