Timu ya Nigeria watangaza bei ya jezi yao watakayoitumia Kombe la Dunia 2018
Ni siku 27 zimesalia michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2018 ianze, huku bara la Afrika likipata nafasi ya kuwakilishwa na mataifa matano ambayo ni Nigeria, Senegal, Misri, Morocco na Tunisia katika fainali hizo zitakazofanyika nchini Urusi.
Kuelekea fainali hizo good news mbalimbali zimeanza kutangazwa na kuna baadhi ya taarifa pia zimewashangaza mashabiki wa soka kutokana na kuna baadhi ya mastaa wa soka ambao tulitegemea kuwaona lakini makocha wa timu zao za taifa wamewaona hawana mchango safari hii.
Ukiachana na hayo ni kuwa jezi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles ambayo imetengezwa na kampuni ya Nike imeanza kununuliwa kwa kasi, Nike tayari wamepokea oda milioni 3 ya kutengenzeza jezi hizo na inakadiriwa hadi Kombe la dunia limalizike watakuwa wametengeneza jumla ya jezi milioni 582 za Nigeria, jezi moja ya Nigeriainauzwa Naira 30,342 ambazo ni zaidi ya Tsh 190000.
Post a Comment