Tangaza Nasi

Wanafunzi wavalishwa maboksi wasipige chabo katika mtihani


Chuo cha The Bhagat Pre-University College kilichopo nchini India kimeomba radhi kwa kitendo chake cha kuwavalisha maboksi Wanafunzi ili kuzuia kupiga chabo wakati wa mtihani wa Chemistry.
Taarifa za wanafunzi wa The Bhagat Pre-University college kilichopo Haveri, Karnataka kuvalishwa maboksi wakati wa mtihani zilienea baada ya kupostiwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook na mmoja wa wafanyakazi katika chuo hicho huku sehemu ya mbele la maboksi hayo yapo wazi.
Msimamizi Mkuu wa Chuo hicho, MB Satish, amesema walitumia njia hiyo kukabiliana na udanganyifu wa kupiga chabo kwa wanafunzi na walifanya hivyo kama jaribio la muda tu kisha waliwatoa maboksi hayo kichwani na kuongeza wapo waliyoyavua baada ya dakika 15 na wengine 20.
“Wapo baadhi ya wanafunzi ambao waliyavua baada ya dakika 15, wengi baada ya dakika 20 na sisi wenyewe tuliwaambia wayaondoe kichani baada ya saa moja.” amesema MB Satish
“Kati ya wanafunzi 72 ni 56 ndiyo walivaa maboksi kama sehemu ya majaribio, walisema wanajisikia vizuri na jaribio hilo na chuo hakijamsumbua mwanafunzi yeyote kuhusu suala la kuvaa maboksi hayo” ameongeza.
Wakuu wa taaluma wa The Bhagat Pre-University College walikimbilia shuleni hapo mara baada ya kusikia kutokea kwa tukio hilo wakiwa na Mkurugenzi wa elimu chuoni hapo nakusema kitendo hicho si ubinadamu.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.