Mbaroni kwa tuhuma za kubaka mtoto wa mwaka mmoja Shinyanga Mjini
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanaume mmoja mwenye umri
wa miaka 26 mkazi wa Ndala Mjini Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto
wa kike mwenye umri wa Mwaka mmoja na miezi 11.
Akizungumza
na Malunde 1 blog, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George
Kyando amesema tukio hilo limetokea Ijumaa Aprili 8,2022 majira ya saa
nane na nusu mchana.
“Tunamshikilia
mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 kwa tuhuma za kumbaka mtoto
wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11”,amesema Kamanda Kyando.
“Mtoto
huyo alibakwa na baba yake wa kambo wakati mama wa mtoto huyo akiwa
ameenda dukani. Mtuhumiwa amemuoa huyo mama akiwa tayari ana mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Kyando.
Habari
kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda
unyama huo alimpeleka mtoto huyo kwa mama mwenye nyumba kisha kumwambia
kuwa mtoto huyo anatokwa damu kwa sababu amejikata kisu.
Post a Comment