Tangaza Nasi

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 02.05.2022:

Mshambuliaji wa England Marcus Ruishford , 24 amehusishwa na habari za kuondoka katika klabu ya Manchester United , lakini atapewa fursa ya kuthibitisha iwapo anapaswa kusalia katika klabu hiyo chini ya mkufunzi mpya Erik ten Hag , ambaye atachukua ukufunzi wa klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard ,29, huenda akasalia katika klabu hiyo. (Sun)

Beki wa Arsenal na raia wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, huenda akahamia katika klabu ya Juventus mwisho wa msimu huu. (Gianluca Di Marzio, via Teamtalk)

Mkurugenzi wa klabu ya Barcelona Mateu Alemany amekana kwamba klabu hiyo ya ligi ya LaLiga imekutana na ajenti wa mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandoowski kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwisho wa msimu huu.. (Movistar, via Goal)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, ambaye ana kandarasi na klabu ya Leicester City hadi 2023, angependelea uhamisho wa kuelekea Uhispania iwapo ataondoka katika klabu hiyo . Real Madrid wanaaminika kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sacha Tavolieri, via Mail)

Manchester United ilimtuma mwanaskauti wake kumtazama kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves akiichezea Wolves katika mechi ambayo klabu hiyo ilishindwa na Brighton 3-0 siku ya Jumamosi. Klabu hiyo ya Old Trafford imedaiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Birmingham Live)

Juventus imempatia ombi kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho kurudi katika klabu hiyo ya ligi ya Serie A , huku kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ikitarajiwa kukamilika 2023. (Todofichajes - in Spanish)

Beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso ni mmoja ya wachezaji ambao klabu ya Barcelona inataka kuwasajili , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akitaka kurudi nchini Uhispania mwisho wa msimu huu . (Fabrizio Romano, via Marca)

Napoli wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 2o Armando Broja, huku mshambuliaji huyo wa Albania akionesha mchezo mzuri akiwa katika mkopo na klabu ya Southampton msimu huu. (Todofichajes - in Spanish)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.