Tangaza Nasi

Miaka 30 Jela kwa kosa la kumbaka Mama yake Mzazi kisa kuyumba kibiashara


Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha Miaka 30 na fidia  ya shilingi Million 1 Mfanyabiashara Kaloli Mkusa mwenye umri wa miaka 30  mkazi wa kijiji cha Msisina kwa kosa la kum-baka MAMA yake mzazi.

Hata hivyo mtuhumiwa yeye pamoja na baba yake Joseph Mkusa ambaye alimuwekea dhamana wametoweka kusikojulikana na hati ya kukamatwa tayari imetolewa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakim Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Emmy Msangalufu amesema mtuhumiwa alifanya Tukio Hilo Tareh 7/05/2021 

Ambapo Mtuhumiwa alikuwa akifanya Biashara zake Tunduma Mkoani Songwe na alirudi akafikia kwa baba yake ambaye anaishi nyumba tofauti na mama Yake kutokana na kutalakiana.

Siku ya Tukio Mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwa mama yake majira ya usiku na kuvunja mlango huku akiwa ameshika panga na kumtisha kumkata kwa kumpiga na ubapa wa upanga.

Licha ya mama Yake kumsihi asifanye hivyo lakini Mtuhumiwa aliendelea na Tukio Hilo mpaka alipomaliza.

Baada ya Tukio Hilo Mama Mzazi alitoa taarifa kwa majirani baadae Serikali ya Kijiji ndipo taratibu za kumkamata zikafanyika. 

Tukio Hilo linasadikiwa Ni kutokana na Imani za kushirikiana kutokana na Biashara za Mtuhumiwa huyo kuyumba.

Kesi hiyo imeendeshwa na wakili wa Serikali Jaquline Nungu pamoja Allice Thomas.

Hata hivyo hati ya kukamatwa ilitolewa Tareh 09/03/2022 lkn mpaka Sasa Mtuhumiwa pamoja na baba yake aliyemuwekea dhamani hawajulikani walipo.

Kwa Mujibu wa Mahakama Kifungo hicho kitaanza kutumika Pindi Mtuhumiwa atakapokamatwa.

 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.