Tangaza Nasi

Zaidi ya Watu tisa wauawa na 90 kujeruhiwa katika shambulio mjini Kabul

media

Zaidi ya watu tisa wameuawa na zaidi ya 90 wengine kujeruhiwa Jumatano hii asubuhi katika mlipuko mkubwa wa bomu lililotegwa katika gari katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, Wizara ya Afya imesema.

Polisi imethibitisha kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na ubalozi wa Ujerumani, katika eneo ambapo kunapatikana ofisi mbalimbali na majengo muhimu ya serikali.

"Ilikuwa bomu lililotegwa katika gari karibu na ubalozi wa Ujerumani, lakini pembezoni mwa eneo la tukio kuna majengo muhimu na ofisi kadhaa. Ni vigumu kusema nani alikua amelengwa," amesema msemaji wa polisi mjini Kabul, Basir Mujahid.

Zaidi ya watu 90 waliojeruhiwa wamesafirishwa hospitalini katika mji wa Kabul, amesema msemaji wa Wizara ya Afya na kuongeza kuwa idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.
 
Moshi mweusi umetandaa eneo la kati la mji wa Kabul na nyumba zilizo kwenye mita kadhaa kutoka eneo la mlipuko zimeharibiwa.hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Msemaji wa kundi la Taliban amesema bado anachunguza.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.