Hali ya sintofahamu imekikumba chama cha ACT-Wazalendo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Hayo yametokea mara baada ya Afisa Habari wa chama hicho, Abbdallah Khamis kushindwa kuelezea undani wa tukio hilo huku ikisemekana baadhi ya wanachama kutoa shinikizo la kukataa uteuzi huo alioteuliwa na Rais.

“Uteuzi huo hata sisi tumeusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo chama kitakaa kikao na Mwenyekiti wetu ili tuweze kuzungumza nae, kani kwasasa siwezi kuzungumzia chochote kwasababu muhusika yupo safarini, hata Zitto naye kasikia kwenye vyombo vya habari hivyo baada ya kikao chama kitatoa tamko,”amesema