Kundi la wanamamgambo wa Islamic State wamekiri kuhusika katika shambulio lililotokea jijini London nchini Uingereza na kuuwa watu saba huku wengine 48 wakijeruhiwa na kupelekwa hospitali.

Aidha, katika shambulio hilo Polisi nchini humo imesema kuwa imewakamata watuhumiwa 12 ambao wanadaiwa kuhusika katika shambulio hilo la kigaidi  ambalo ni baya kutokea kwa nchi ya Uingereza.

Hata hivyo, ulinzi umeimarishwa na msako mkali dhidi ya wahusika unaendelea jiji humo huku bado kukiwa na hofu kubwa ya mashambulizi mengine kutoka kwa magaidi hao jijini London.