Benjamin Mkapa: Natambua ugumu wa kazi yangu
Wakati ambapo mazungumzo baina ya Wurundi yakiwa
bado yamesimama, hotuba ya Mwezeshaji katika mazungumzo hayo rais
mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa alioitoa mbele ya wakuu wa nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Mei 20 imeendelea kugonga
vichwa vya habari.
Katika hotuba hiyo, Benjamin Mkapa, ambaye ni mara chache kuelezea kuhusu kazi yake, alielezea matatizo yaliyojitokeza wakati wa kazi ya ke jiyo ya kuwakutanisha wadau wote katika mgogoro wa Burundi. Benjamin Mkapa alisema sehemu moja ya upinzani hauna imani naye na serikali ya Burundi haina utashi wa kushiriki katika mazungumzo, kazi si rahisi kwa mazungumzo baina ya Warundi, ameongeza bwa Mkapa.
Nchini Burundi, tangu kuanza kwa mgogoro huo wa kisiasa mwezi Mei mwaka 2015, mazungumzo ya kisiasa yanaonekana kushindikana. Tangu mwaka 2016, rais wa mtaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa anahakikisha kuwa ana kazi kubwa ya kuzikutanisha pande hasimu katika mazungumzo hayo chini ya uangalizi wa upatanishi wa rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. Tangu wakati huo alikutana mara tatu na makundi mbalimbali ya Warundi katika mji wa Arusha, lakini bila matokeo halisi kwa sasa.
Ni mwaka mmoja sasa tangu kuanza kwa kazi yake.Benjamin Mkapa hajaweza kukwakutanisha kwenye meza moja ya mazungumzo wahusika wakuu katika mgogoro unaoendelea nchini Burundi. Alikutana kwa nyakati tofauti na makundi mbalimbali, na kukusanya maoni yanayoonekana magumu kwake kukubaliana nayo.
Serikali inaendelea kusema kuwa hali ni shwari na nchi ina amanii, huku ikiendelea kusisitiza kuwa mazungumzo yanapaswa kufanyika nchini Burundi na imeahidi kufanya marekebisho ya baadhi ya ibara za katiba. Jambo ambalo linafutiliwa mbali na upinzani, ambao unasema kuwa hakuan usalama nchini humo na watu wanaendelea kukamatwa kiholela, huku kukishuhudiwa visa mateso na mauaji.
Benjamin Mkapa ameitaka serikali ya Burundi kuonyesha nia njema kwa kushiriki mazungumzo hayo na hasa kufuta hati za kukamatwa zilizotolewa dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa mashirika ya kiraia, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa na kukubali makundi ya waasi kushiriki katika mazungumzo.
Benjamin Mkapa amesema kuwa anasikitishwa na kuvuja kwa baadhi ya taarifa, huku akisem akuwa baadhi ya nyaraka zake zimekua zikiwasilishwa kwa sekretarieti ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Post a Comment