Tangaza Nasi

Polisi ya Uingereza yataja magaidi wawili waliohusika na shambulio London

 
Polisi ya Uingereza iliwataja watu wawili kati ya watatu waliohusika na shambulizi la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini London nchini Uingereza na kusababisha vifo vya watu 7 na kuwajeruhi wengine 48.

Watu hao ni pamoja na Khuram Shazad Butt, mwenye umri wa miaka 27, Mwingereza aliyezaliwa nchini Pakistan na anajulikana na polisi, na Rachid Redouane, mwenye umri wa miaka 30, ambaye alijitambulisha kama ana uraia wa Libya na Morocco.

Polisi nchini Uingereza ilisema kuwa hakukua na taarifa zilizoonyesha kuwa alikua akiandaa shambulio hilo.

Rachid Redouane hakua anajulikani na polisi. Vyanzo vya polisi katika mji wa Dublin vilieleza kwamba siku ya Jumamosi jionialikua na kitambulisho cha uraia wa Irland na aliishi katika mji wa Dublin kati ya mwaka 2014 na 2016.

Wakati huo huo polisi ya Uingereza ilisema kuwa inaendelea na uchunguzi ili kumtambua gaidi wa tatu. Polisi pia ilijizuia kusemakuhusu ushahidi wa uliotolewa na watu wengi msimamo mkali ulioonyeshwa na mmoja wa magaidi na kuona mara nyingi viongozi walipewa taarifa kuhusu kutokea kwa hali hiyo na hawakuweza kuzuia chochote.

Waziri Mkuu Bi.Theresa May amesema nchi hiyo bado inakabiliwa na tishio la ugaidi, na hivyo maafisa wa usalama wanafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuhakikisha kuwa shambulizi lingine halitokei tena nchini humo.

Kundi la kigaidi la Islamic State limejigamba kutekeleza shambulizi la pili la kigaidi kwa kipindi cha miezi miwili.

Wanasiasa wanarejelea kampeni zao kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi wiki hii, ushindani mkali ukitarajiwa kuwa kati ya chama cha Labour na Conservative.

Polisi wanasema wanawashikilia watu 11 kwa mahoajino zaidi kuhusu shambulizi hilo, huku rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisema Paris, itaendelea kusimama na Uingereza katika vita dhidi ya ugaidi.

Watu hao walipoteza maisha baada ya kugongwa na gari katika daraja maarufu jijini London na kuwadunga visu watu wengine, huku washambuliaji hao wakipigwa risasi na kuuawa na polisi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.