Chama cha ANC Waanza Kumpinga Rais Zuma..Wataka Achunguzwe kwa Rushwa..!!!
Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimetaka
vyombo vya dola kuchunguza barua pepe zilizoibua kashfa ya rushwa kati
ya familia ya Rais Jacob Zuma na familia ya wafanyabiashara wakubwa
nchini humo ya Gupta.
Kwa mujibu wa ANC wameeleza kuwa tuhuma hizo nzito zinapunguza imani na
heshima ya serikali yake, hivyo kashfa hizo hazipaswi kuvumilika au
kupuuzwa.
Baadhi ya vigogo wa ANC waliungana na upande wa upinzani hivi karibuni
wakitaka Rais Zuma ajiuzulu kutokanana na kuandamwa na kashfa za rushwa.
Kura za kumtetea zilitosha kumpa nafasi kiongozi huyo kuendelea
kuliongoza taifa hilo, huku akiomba radhi kwa kutumia fedha za serikali
kukarabati jumba lake kinyume cha sheria.
Hata hivyo, wanasheria wa Zuma wameendelea kupinga vikali kashfa hizo
kwa madai kuwa barua pepe zilizovujishwa zilikuwa na mkakati wa kisiasa
nyuma yake dhidi ya mteja wao.
Tuhuma za rushwa kati ya familia ya Rais Zuma na familia ya mabilionea
ya Gupta zilidai kuwa familia hiyo ya kitajiri imekuwa na nguvu kubwa
katika upangaji wa nafasi za uteuzi za Serikali hiyo kwa kutumia uwezo
wake wa kifedha.
Post a Comment