Tangaza Nasi

Congamano la kimataifa kuhusu msaada kwa wakimbizi kufanyika Uganda


Kongamano la siku mbili la Kimataifa kutafuta njia za kuwasaidia wakizmbi nchini Uganda linaanza leo jijini Kampala. Uganda inawapa hifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani kama vile Sudan kusini, Rwanda, Burundi na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ndio mgeni rasmi katika kongamano hilo ambalo mwenyeji wake ni rais Yoweri Museveni.

Wajumbe na watalaam mbalimbali pia wapo jijini Kampala kujadili suala hili.

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Uganda kwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi Milioni 1.2 kutoka Sudan Kusini , Burundi , Rwanda , Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini inaelemewa na gharama za kuwasaidia.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune


Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.