Tangaza Nasi

Trafiki Wawili Wauawa Kibiti....

Askari Polisi wawili wa kikosi cha usalama wa barabarani wilayani Kibiti ambao majina yao bado hayajatambulika wamepigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.

Mbali na kupigwa risasi, pia watu hao wamechoma moto gari moja na pikipiki moja za askari hao kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema anafuatilia.

Tukio hilo limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari polisi wanane kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa wakitoka doria katika Kijiji cha Jaribu.
 

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.