Tangaza Nasi

Dunia yatakiwa kuwalinda watu wenye Albinism

Dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu watu wenye Albinism.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International jumla ya watu 18 wenye albinism waliuawa nchini Malawi na watano walitekwa nyara toka mwezi Novemba mwaka 2014.

Hata hivyo nchi kadhaa barani Afrika zimefanikiwa kudhibiti mauaji ya watu wenye Albinism wanaouawa kwa imani za kishirikina, vitendo ambayo wakati fulani vilikuwa vimekithiri kwenye ncui za Malawi, Tanzania na Msumbiji.

Wanaharakati wanatumia siku hii kuzikumbusha Serolali na watu, umuhimu wa kuwakubali watu hao na kuwaona sehemu ya jamii.

Ziada Ally Nsembo ni Mwanaharakati na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama Albino nchini Tanzania, taifa ambalo Albino wamekuwa wanaishi kwa wasiwasi kutokana na visa vya kushambuliwa na hata kuuawa kwa imani potofu.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.