Tangaza Nasi

Polisi wengi waongezwa katika jimbo la upinzani Venezuela

Serikali ya Venezuela kupitia wizara ya mambo ya ndani imeongeza imewatuma apolisi wengi katika jimbo la Miranda, ambalo linaongozwa na kiongozi wa upinzani nchini humo Henrique Capriles.

Jimbo hili linakabiliwa na vitendo vya ukiuwaki mkubwa wa haki za binadam, kwa mujibu wa serikali.
Miranda amabayo ni sehemu ya mji mkuu Caracas ni miongoni mwa sehemu zenye maandamano makubwa dhidi ya Rais Nicolas Maduro.

Henrique Capriles ameeleza kwamba kitendo cha wizara kuongeza polisi katika jimbo lake ni masuala ya siasa zaidi ya ulinzi.

Serikali imejitetea ikisema kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadam katika eneo hilo.
Machafuko nchini Venezuela yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 60 ambao waliuawa katika maandamano yaliyoanza miezi miwili iliyopita, ambapo waandamanji wamekua wakidai rais Nicolas Maduro ajiuzulu.


Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.