Klabu ya Sevilla ya Hispania ipo katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji wa mabingwa wa soka wa England (Chelsea), Michy Batshuayi.

Meneja mpya wa Sevilla Eduardo Berizzo anatajwa kuongoza vita ya usajili wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji, ambaye msimu uliopita alipata wakati mgumu wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Antonio Conte.

Berizzo ameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya Hispania, anaamini uwezo wa Batshuayi utaweza kufanikisha mipango aliyojiwekea kwa msimu wa 2017/18 ambao utaanza rasmi mwezi Agosti mwaka huu.

Katika hatua nyingine mshambuliaji wa AC Milan Carlos Bacca, naye ameorodheshwa katika mipango ya meneja huyo kutoka nchini Argentina, na inasmeekana wakati wowote huenda ofa yake itumwa mjini Milan nchini Italia.