Tangaza Nasi

EU kuipa Uganda Euro Milioni 85 kushughulikia wakimbizi


Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa Euro Milioni 85 kwa nchi ya Uganda kusaidia kuwashughulikia zaidi ya wakimbizi Milioni moja nchini humo.

Ahadi hii imetolewa katika kongamano la siku mbili kuhusu wakimbizi linalomalizika leo jijini Kampala.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amewatembelea wakimbizi wa Sudan Kusini Kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka machafuko kumalizika katika taifa hilo ili kuepusha raia wa nchi hiyo kuyakimbia makwao.

Kupitia kongamano hili, Uganda inatarajiwa kupata Dila Bilioni 2 kusaidia kuwahifadhi wakimbizi hao.

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Uganda kwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi Milioni 1.2 kutoka Sudan Kusini , Burundi , Rwanda , Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini inaelemewa na gharama za kuwasaidia.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.