Tangaza Nasi

EU kusaidia kupambana na ugaidi ukanda wa sahel

Jeshi la Mali na wapiganaji wa zamani kutoka makundi mbalimbali wakipiga doria, Gao Februari 23, 2017. (Picha ya zamani).

Umoja wa Ulaya umekubali kutoa zaidi ya dola milioni hamsini kwa muungano mpya wa pamoja barani Afrika wa nguvu za kijeshi kutoka mataifa matano katika eneo la Sahel, kuunda jeshi la pamoja kupambana na ugaidi Kaskazini mwa bara la Afrika.

Majeshi hayo yataundwa katika vikundi vidogo vidogo kutoka nchi tano za Afrika Magharibi ambazo ni Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger na Chad kwa lengo la kupambana na ugaidi Kaskazini mwa bara la Afrika, hasa wanamgambo wenye itikadi kali za kidini.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Mali , Abdoulaye Diop ametangaza kuwa jeshi hilo litaundwa na wanajeshi 15,000 na polisi, ongezeko la mipango ya awali kwa askari elfu tano.

Duru kutoka muungano huo zinasema kuwa utekelezaji wa mpango huo utakamilika hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Makundi mbalimbali ya wanamgambo wenye silaha yameendelea kuhatarisha usalama wa raia wa ukanda huo na kusababisha kiwango cha usalama kuendelea kushuka,.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na hali ya usalama mdogo inayosababishwa na makundi haya.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.