Mamlaka ya rais wa Brazil Michel Temer hatarini
Rais wa Brazil Michel Temer ambaye anashtumiwa
kujihusisha na rushwa, anakabiliwa kuanzia Jumanne hii Juni 6 na kesi
hatari, pamoja na kurejelea hukumu ya Mahakama Kuu ya Uchaguzi (TSE)
ambayo inaweza kumuondoa mamlakani.
Majaji saba wa mahakam hii TSE wanaweza kuamua kufuta uchaguzi wa rais wa mwaka 2014 ambao ulimfikisha madarakani Dilma Rousseff kama rais wa nchi hiyo na Bw Temer kama makamu wa rais.
Michel Temer alichukua wadhifa wa rais mwaka mmoja uliopita, baada ya Dilma Rousseff kutimuliwa kwa kosa la utumiaji mbaya wa mali ya umma.
Rais Michel Temer na aliekuwa rais Dilma Roussef
Katika kesi ya kutothibitisha uchaguzi wa mwaka 2014, mahakama itaamua kama Bw Temer atajiuzulu mara moja au unaweza kusalia kwenya wadhifa huo mpaka kumalizika kwa mchakato mzima wa kesi hiyo mbele ya mahakam hiyo ya TSE na hata mbele ya Mahakama Kuu.
Katika hali zote mbili, Brazil inaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu kwa kipindi chote hiki.
Kesi hii ambayo inaanza Jumanne hii saa 7:00 usiku saa za Brazil (sawa na saa 4:00 usku saa za kimataifa) inahusu makosa katika ufadhili wa kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2014.
Utaratibu unaweza kuongezwa kwa wiki kadhaa, kwa mujibu wa wachambuzi na wataalam wa sheria za Uchaguzi waliohojiwa na shirika la habari la AFP.
Post a Comment